Taarifa hiyo imetolewa Januari 28, 2022 na Kaimu Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Eng. Aswile Mwasaga kwenye Mkutano wa Baraza la Madiwani Kufuatia maswali ya baadhi ya Madiwani walipotaka kufahamu hatua waliyofikia juu ya ukarabati na ufunguaji wa barabara katika maeneo yao kupitia fedha Bil. 1.5 iliyotengwa na Serikali.
Eng. Mwasaga amesema kuwa fedha hizo zimetolewa kwa ajili ya kufanya marekebisho kwenye barabara ya Madangwa-Sudi, kufungua, kuchonga, kuweka kifusi na makaravati katika barabara ya Mnolela - Mbuta, lakini pia fedha hizo zitatumika kuweka boksi karavati katika daraja la Mtumbya. Pia, Serikali imetoa Mil 500 kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya NAHUKAHUKA-Chiuta-Nambahu, Hingawali-Navanga pamoja na Navanga -Nachunyu.
Ameongezea kuwa utekelezaji wa mikataba ya fedha hizo umeanza mwezi Disemba na kwamba baadhi ya wakandarasi ikiwa ni pamoja na Mkandarasi wa barabara ya Mtumbya tayari ameanza kazi ya kuweka karavati na wakati huo huo Madangwa - Sudi zoezi la uchongaji kwa sehemu korofi unaendelea, aidha kwa upande wa barabara ya Mnolela - Mbuta tayari Mkandarasi amepeleka vifaa kwa ajiri ya ujenzi wa barabara hiyo.
Kwa hatua nyingine kupitia Baraza hilo, Kaimu Afisa Kilimo Ndg. Selemani Kambi alitolea ufafanuzi juu ya swali la Diwani wa Kata ya Nachunyu Mhe. Chipatu Omary alipohoji kuhusu mikakati ya Halmashauri kupitia Idara ya kilimo kutatua tatizo la panya lililopo katika kata ya Namangale. Ndg. Kambi alisema kuwa Idara ya Kilimo tayari imeandika barua kwa Katibu Tawala Mkoa wa Lindi ili kuomba sumu itakayosaidia kuua panya wanaoharibu mazao bila kuleta madhara yoyote kwa binadamu. Lakini pia Kambi alitumia fursa hiyo kuwashauriwa wakulima kutumia mbegu za muda mfupi zinazostahimili ukame kutokana na uwepo hali ya uchache wa mvua katika maeneo mengi.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Lindi Ndg. Thomas Safari ametoa msisitizo kwa uongozi wa Halmashauri kuwatumia Maafisa Tarafa waliopo ili kupunguza tatizo la uhaba wa watumishi kwani miongoni mwao kuna wanasheria, walimu nakadharika.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.