Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa ( TAKUKURU) Mkoa wa Lindi Disemba 07, 2021 imekabidhi Mwongozo wa Wawezeshaji wa Kufundisha vijana wa Skauti kuhusu kuzuia na kupambana na Rushwa kwa ngazi ya Wilaya- Mtama. Mwongozo huo amekabidhiwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. Georege Emmanuel Mbilinyi Ofisini kwake kutoka kwa Mkuu wa TAKUKURU Mkoa wa Lindi Abnery Mganga na Kamishina wa Skauti Bi. Fidea Nnunduma.
Mwongozo huo unakusudia kuwaongoza wawezeshaji ili wawafundishe vijana wa Skauti kuwa waadilifu, wawajibikajina wazalendo kuanzia ngazi yao binafsi, familia, shuleni, jamii na Taifa kwa ujumla. Aidha kupitia mafunzo mbalimbali watakayopatiwa yatasaidia kubadilisha nadharia za mada za mapambano dhidi ya Rushwa watakazojifunza zitawawezesha kuziweka katika vitendo ikiwa ni pamoja na kutojihusisha na vitendo vya Rushwa, kutoa taarifa za vitendo vya Rushwa lakini pia kuhoji vitendo vinavyoashiria Rushwa kwa ngazi zote.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama Ndg. Mbilinyi amewapongeza TAKUKURU kwa kuwa na mkakati wa ushirikishwaji wa kuzuia Rushwa kuanzia ngazi za chini huku akiongezea kuwa kwa kufanya hivyo itasaidia kupunguza tatizo la Rushwa nakuahidi kutoa ushirikiano katika utekelezaji wa Mkakati huo.
Huu ni Mkakati wa TAKUKURU na Skauti ambao pia ni utekelezaji wa Mkakati wa Taifa Dhidi ya Rushwa na Mpango wa Utekelezaji Awamu ya Tatu ( National Anti-Corruption Strategy and Action Plan Phase III – NACSAP III) wa mwaka 2017/18-2021/22 unaosisitiza ushirikishwaji katika mapambano dhidi ya Rushwa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.