Shirika la Heart to Heart na Wakuu wa idara na vitengo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama wamefanya kikao cha kwanza cha uwezeshaji wa mradi wa usafi wa mazingira, utekelezaji wa mradi huo utafanyika katika kata tatu ambazo ni kata ya Mtama, Sudi na Nyangamara ambapo wananchi 122,823 watafikiwa na mradi huo, kikao hiko kimefanyika leo tarehe 18 Aprili 2024 katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri.
Aidha mradi huo utalenga kuchimba visima 14 vya maji katika vituo vya kutolea huduma za afya, kutoa elimu na kuhamasisha ujenzi wa vyoo bora na kuelimisha jamii kuhusu umuhimu wa kunawa mikono baada ya kutoka chooni.
Yote hayo yanatokana na mahusiano mazuri kati ya Halmashauri na Heart to Heart, ambapo hapo nyuma Heart to Heart iliwezesha kampeni ya Nyumba ni Choo kata ya Namangale na Nyangao, walitoa fedha kwaajili ya kupambana na UVIKO 19, walitoa gari aina ya Prado, walijenga vyoo 11 na walijenga visima vya maji katika Shule na Zahanati.
Katika kikao hicho Ndugu Abraham Msofe katibu wa mradi aliishukuru Halmashauri kwa ushirikiano mzuri kuwezesha Mafanikio ya miradi iliyopita pia aliongeza kuwa watashirikiana na Masharika mengine kama DMDO ili kufanikisha mradi huo.
Matokeo ya mahusiano mazuri kati ya Serikali na mashirika binafsi yanadhihilika katika Halmashauri ya Mtama, Mwisho Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri alilishukuru shirika hilo na alisema kuwa mradi ukawafikie wananchi pia aliomba shirika hilo kufungua Ofisi Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.