Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi Disemba 31, 2021 ametoa salamu za mwaka mpya 2022 kwa watumishi wa Halmashauri, wananchi wa Mtama pamoja na Watanzania wote kwa ujumla
Katika salamu zake Mbilinyi ameishukuru Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka fedha katika Halmashauri hiyo Tsh. Bil 19.4 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwenye sekta ya Elimu, Maji, afya na barabara.
Amesema kwenye sekta ya afya Mhe. Samia amepeleka shilingi million 500 kwa ajili ya ujenzi wa wodi tatu ambazo ni wodi ya wanawake, wanaume na watoto, million 800 ujenzi wa miundombinu mingine katika hospitali ya Wilaya iliyoko Kata ya Kiwalala 250 kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya cha Mtama na kwamba ujenzi unaendelea ukiwa kwenye hatua mbalimbali.
Katika hatua nyingine Mhe Rais amepeleka billion 1.8 ujenzi wa madarasa kwa shule za msingi na sekondari lakini pia umaliziaji wa madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi. Vilevile Serikali imetenga billion 13.7 kukamilisha miundombinu ya maji huku billion 1.4 kwa ajili ya ukarabati na kufungua barabara ambazo zikisahaulika ndani ya Halmashauri.
Aidha Mbilinyi ametoa wito kwa wananchi kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika mwaka 2022 ili kuirahisishia Serikali kutoa huduma kwa wananchi wake. Sambamba na hilo amewahimiza wazazi kuwaandikisha watoto wao shuleni kwani madarasa yapo yakutosha.
"Nawatakia heri ya mwaka mpya watumishi wa halmashauri, wananchi wa MTAMA na watanzania kwa ujumla. 2022 kazi iendelee" George Mbilinyi Mkurugenzi Halmashauri ya Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.