Zoezi la usajili wa watoto wenye umri chini ya miaka mitano limefanyika katika ukumbi wa Chekechea Kanisani katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Siku ya tarehe 22 Juni 2021. Mafunzo hayo yameratibiwa na RITA na kuhudhuriwa na watumishi mbalimabi wakiwemo Madiwani, Watendaji wa kata pamoja na Wasimamizi wa vituo vya afya kutoka Jimbo la Mtama na Mchinga
Akifungua mafunzo hayo Kaimu Tatibu Tawala wa Wilaya ya Lindi Bi Herieth Karua amebainisha umuhimu wa zoezi hill kwa kuwa Cheti cha kuzaliwa kinasaidia katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, kusafiri pamoja na harakati za kutafuta ajira. Aidha kaimu Katibu Tawala Wilaya ya Lindi ameongezea kuwa vyeti hivyo vinatolewa bure bila malipo yoyote na kusisitiza umakini kuhusiana na udanganyifu wa taarifa zinazotolewa na wahusika na kwa kufanya hivo ni kosa kisheria kwa mujibu wa kifungu cha sheria ya vizazi na vifo kifungu Namba 29. kifungu kidogo cha 3 kinachosema ni kosa kisheria kutoa taarifa za uongo.
Kwa upande wake Mratibu wa zoezi hilo kutoka RITA Mkoa wa Lindi Bi Halima Ramadhani Mumwi ameelezea lengo la zoezi ikiwa ni pamoja na kutoa hamasa na kuwakumbusha watoa huduma za afya kuhusu umuhimu wa vyeti vya kuzaliwa, aidha amesema kuwa matarajio ya zoezi hilo ni kuhakikisha kila mtoto mwenye umri chini ya miaka mitano anapata cheti cha kuzaliwa.
Zoezi la usajili wa watoto walio na umri chini ya miaka mitano lilianza mwaka 2017 kwa lengo la kurahisisha upatikanaji wa vyeti vya kuzaliwa na huu ni muendelezo wa kampeni hiyo ambapo matarajio ni kuhakikisha watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wanapata vyeti vya kuzaliwa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.