Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainabu Telack leo tarehe 8 Machi 2024 ameongoza kilele cha sherehe ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani, maadhimisho hayo kimkoa wa Lindi yamefanyika katika uwanja wa Ilulu uliopo manispaa ya Lindi.
Katibu tawala wa mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zuwena Omary alisema anawashukuru wanawake wote kutoka Halmashauri mbalimbali ndani ya Mkoa kwa kufanya mambo mbalimbali kama vile kufanya usafi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya, kuchangia damu na kurudisha shukran kwa jamii aliongeza kuwa mambo yaliyofanywa na taasisi mbalimbali kuelekea kilele ya siku hiyo yameongeza ufahamu kwa jamii kuhusu siku ya wanawake duniani.
Mheshiwa Telack alisema kuwa katika maadhimisho hayo jamii inatakiwa kuelewa umuhimu wa elimu kwa wanawake, wanawake watimize jukumu lao la msingi la kutunza familia aliongeza kuwa Tanzania kupitia Mheshiwa Rais Daktari Samia Suluhu Hassan imeondoa dhana ya kwamba wanawake hawawezi kuongoza hivyo akuwaomba wanawake kujitokeza kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi ujao wa Serikali za mitaa.
Kwaniaba ya Wanaume Mstahiki meya wa Lindi alisema kuwa bila wanaume hakuna wanawake hivyo wanawake wanapaswa kushirikiana vyema na wanaume katika kufikia malengo ya familia na taifa.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi aliwashukuru viongozi wa Serikali, Chama Cha Mapinduzi, Dini na Taasisi mbalimbali pamoja na wote walioshiriki katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani kwa mkoa wa Lindi. Mwisho kwa Halmashauri ya Mtama Sherehe hizo zitaendelea leo Usiku katika ukumbi wa Halmashauri ambapo Mkurugenzi Mtendaji Ndugu George E. Mbilinyi ameahidi kuunga mkono sherehe hizo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.