Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainabu Telack amewataka wananchi wa Mkoa huo kulima mazao ya Chakula ili kujikinga na njaa akisisitiza Lindi imebarikiwa maeneo makubwa na ardhi yenye rutuba hivyo si vizuri kutegemea chakula kutoka mikoa mingine.
Aidha kutokana na kasumba ya wananchi kujikita zaidi katika kilimo cha biashara Mkuu wa Mkoa aliwataka Maafisa Kilimo kuhakikisha kuwa kila kaya inalima mazao ya chakula kama vile mahindi, mpunga, mtama, mihogona viazi.
Mwisho Mkuu wa Mkoa amewataka wananchi wanaoishi karibu na mito hasa mto Lukuledi kuwa makini pindi wanapovuka mito hiyo kwasababu usalama wa mwanachi unaanza na mwananchi mwenywewe pia alisema barabara zilizo alibiwa na mvua zitarekebishwa, Mkuu wa Mkoa aliyasema hayo jana tarehe 17, Februari 2024 katika kikao chake na wafanyakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.