Katibu Tawala Mkoa wa Lindi Mama Rehema Madenge ametoa agizo kwa mafundi, kamati pamoja na wasimamizi wa ujenzi wa madarasa ya UVIKO 19 kuhakikisha wanaongeza kasi na kutumia jitihada za ziada ili kuendana na lengo la Serikali la kukamilisha madarasa hayo ifikapo Desemba 15, 2021. Agizo hilo amelitoa Novemba 30, 2021 akiwa katika ziara yake ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kukagua maendeleo ya ujenzi wa miradi hiyo katika shule mbalimbali.
Bi. Rehema amewataka Wakuu wa shule zenye miradi hiyo kuweka miundombinu ya umeme au taa katika eneo la kazi zitakazowasaidia mafundi kufanya kazi usiku na mchana. Aidha amewahimiza mafundi kuongeza nguvu kazi kwa lengo la kukamilisha kwa wakati majengo hayo.
Katika hatua nyingine akiwa kwenye shule ya sekondari Mtua, Katibu Tawala aliwapongeza mafundi, kamati pamoja na wasimamizi kwa kufikia hatua ya boma huku akiwataka kutoridhika na pongezi hizo na badala yake wanatakiwa kuongeza bidii ya kuhakikisha wanafikia hatua ya rinta hadi kufikia Ijumaa ya tarehe 3 Decemba 2021.
Hatua ya mwanzo ya boma na mafundi wakiendelea na kazi shule ya sekondari Mtua
Kwa upande wake Afisa Elimu Mkoa wa Lindi Ndg. Vicent Kayombo aliongezea kuwa ili kufikia lengo la Serikali ni lazima kazi ifanyike kwa ushirikiano wa hali ya juu na kwamba wasimamizi wote wanatakiwa kuwa kwenye vituo vyao vya kazi walivyopangiwa
Mama Rehema Mdenge ameagiza hadi kufikia Desemba 3,2021 majengo yote yanayojengwa ndani ya Halmashauri ya Mtama yawe katika hatua ya rinta huku akiongezea kuwa madarasa hayo yawe kwenye ubora unaoendana na thamani ya fedha lakini pia yanatakiwa kukabidhiwa yakiwa na madawati.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.