Hamasa hiyo imetolewa na wawakilishi kutoka Chuo Cha Usafirishaji Cha Taifa NIT katika nyakati tofauti Kwa wanafunzi wa shule za sekondari za Mtama na Nyangao High school tarehe 23 Februari 2022 na kusisitiza kuwa kusoma masomo ya sayansi kutawafungulia fursa mbalimbali za kimasomo pamoja na ajira lakini pia itasaidia kupunguza uhaba wa wataalamu kwenye sekta tofautitofauti.
Chuo hicho kinaendesha kozi mbalimbali zikiwemo za urubani, unahodha wa Meri pamoja na uundaji na matengenezo ya boti. Aidha chuo hicho kina program ya kutoa hamasa katika shule za sekondari ili wanafunzi hususani wa kike kupenda kusoma masomo ya sayansi kwa ikiwa ni sehemu ya kutoa fursa Kwa vijana hao kupata nafasi ya kusoma katika chuo hicho kwani Kila kozi inahitaji usome masomo ya sayansi.
Kiujumla vijana hao wamefurahishwa Kwa ujio wa wawakilishi hao na hamasa waliyoipata na kuahidi kusoma na kuweka mkazo katika masomo hayo ukizingatia miundombinu ya maabara ineboreshwa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.