Waziri Mkuu wa Tanzania mh Kasim Majaliwa Majaliwa jana amezindua mradi wa uunganishwaji wa umeme katika gridi ya taifa kwa mikoa ya Lindi na Mtwara na kuagiza kuunganisha umeme huo katika Taasisi zote za umma
Akizungumza na baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Lindi na Mtwara waliohudhuria hafla hiyo mara baada ya uzinduzi Majaliwa alisema kuwa uunganishaji wa mikoa hiyo katika Gridi ya Taifa sasa kutaifanya mikoa hiyo kuwa na umeme wa uhakika sambamba na kufunguka kiuchumi
Alisema serikali imedhamilia kumaliza kabisa tatizo la umeme kwa nchi mzima na kwamba mkakati uliopo kwa sasa ni kuendelea kuboresha miundombinu ya zamani sambamba na kuanzisha miradi mipya ya kufua umeme
Alisema sasa tatizo la kukatika kwa umeme kwa mikoa hiyo mara kwa mara litakuwa limemalizika kwani baada ya kuungaanisha mikoa hiyo sasa itakuwa inatumia zaidi ya njia tatu yaani kama njia moja itapata itilafu njia nyingine itaweza kusaidia
“nlipoingia hapo ndani wataalamu wameniambia kuwa umeme huo kwa sasa wameuweka kwenye njia ambazo kama njia moja ikipata tatizo njia nyingine itaweza kutatua tatizo na umeme hutaweza kukosekana kama njia moja Haitakuwa kuwa na tatizo hiyo ni wajibu wa kila Mwananchi kufurahia umeme huu
Aidha Majaliwa pia aliwahasa wananchi wa Mikoa ya Lindi na Mtwara kuutumia umeme huo katika shughuli za kiuchumi kama vile kuanzisha viwanda vidogo vidogo ili waweze kujiongezea kipato
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.