Aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg Samwel Warioba Gunzar leo tarehe 14 Agosti 2021 amekabidhi rasmi madaraka kwa Mkurugenzi mteule Ndg George Mbilinyi kufuatia uteuzi wa Wakurugenzi wa Halmaahauri uliofanywa na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluh Hassani tarehe 01 Agosti 2021, ambapo Ndg Samwel Gunzar amebadilishiwa kituo cha kazi na kupelekwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara huku Ndg George Mbilinyi akiteuliwa kwa mara ya kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama mkoani Lindi.
Hafla ya tukio la makabidhiano hayo imefanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Yusuph Abdallah Tipu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wa Wilaya ya lindi Mh. Othman Ongonyoko, Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg George Mbilinyi na wakuu wa idara na vitengo mbalimbali.
Ndg. Samwel Gunzar alitumia fursa hiyo kutoa neno la shukurani kwa watumishi wa Mtama kwa ushirikiano waliompa katika kipindi chake chota cha uongozi na kuwaomba waendelee kuwa na moyo huo hata kwa kiongozi aliyeteuliwa sasa. Aidha amesisitiza kuwa na usimamizi nzuri wa mapato na matumizi ili kuhakikisha miradi mbalimbali ya kimaendeleo inakamilika kwa wakati. Sambamba na hilo amemtakia kila la kheri Mkurugenzi mpya katika utekelezaji wa majukumu yake na kuahidi kumpa ushirikiano wa kiutendaji.
Akipokea taarifa ya makabidhiano Ndg George Mbilinyi alipata nafasi ya kumshukuru Mkurugenzi aliyeondoka kwa kuweza kutenga muda wake na kuja kukamilisha tukio hilo. Vilevile Mkurugenzi mpya ameongezea kuwa ili kufikia malengo ya kuifanya halmashauri kuwa bora ni lazima watumishi wawe tayari kujitoa na kufanya kazi kwa bidii.
"Katika taasisi yoyote ile hakuna kitu kizuri kama kufanya kazi as a team". Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Yusuph Abdallah Tipu alipopata nafasi ya kuzungumza Katika tukio hilo wakati nae Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi wilaya Mh. Othman Ongonyoko alitumia nafasi hiyo kusisitiza juu ya suala la kufuata maadili ya kazi na ushirikiano wa kisiasa ili kufikia malengo. Kwa upande wa mwakilishi wa wakuu wa idara Afisa Elimu Msingi Mwl. Dastan Ntauka alipata nafasi ya kuzungumza kwa niaba yao na kusema kuwa wako tayari kufanya kazi kwa umoja katika nyanja zote za utendaji.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.