Kampeni hiyo imezinduliwa Kimkoa tarehe 11 Januari 2022 kwa Mikoa ya Lindi na Mhe Shaibu Ndemanga Mkuu wa Wilaya ya Lindi katika kijiji cha Mnolela kilichopo ndani ya Halmashauri ya Mtama
Katika hotuba yake Mhe. Ndemanga aliwasitiza wananchi kuona umuhimu wa kupata elimu ya matumizi bora ya mbolea na kwamba wanatakiwa kuwatumia wataalamu wa kilimo ngazi za Kata na Vijiji ili waweze kupata ushauri wa njia bora ya matumizi ya mbolea hali itakayosaidia kukifanya kilimo kiwe chenye tija na endelevu. Mwisho aligawa mbegu na mbolea kwa baadhi ya wakulima na kuonesha kwa vitendo namna ya kupanda na kutumia mbolea hizo kwenye shamba moja la mfano darasa.
Mamlaka ya Udhibiti wa Mbolea Tanzania, imeendelea kutoa elimu ya matumizi bora ya mbolea kwa vikundi mbalimbali na kuandaa kilimo darasa mahsusi katika kutoa elimu na kujenga uwezo utakaosaidia wananchi wengine kutekeleza kilimo kwa mfano na kujenga hari ya kupata mafanikio makubwa katika kilimo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.