Mbunge wa Jimbo la Mtama lililopo Halmshauri ya Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi Mh. Nape Mosses Nnauye ametoa pongezi kwa uongozi mara baada ya kutembelea eneo lililotengwa kwa ajili ya ujenzi wa kituo cha afya katika kijiji cha Mvuleni Kata ya Mtama, amesema ameridhishwa na kitendo cha Halmashauri kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa huduma mbalimbali za kijamii huku akitoa wito kwa uongozi wa Halmashauri hiyo kuendelea kutoa hamasa kwa wananchi kujitokeza kushiriki shughuli mbalimbali za kujitolea pindi ujenzi wa kituo hicho utakapoanza ”Kwanza nikupongeze Mkurugenzi na timu yako nimefurahishwa sana na jambo hili eneo ni zuri na linafikika kwa urahisi litatuondolea adha na changamoto kwa wananchi wetu kutembea umbali mrefu kufuata huduma za afya ”alisema Nape Mbunge wa Jimbo la Mtama.
Aidha kwa pande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmshauri hiyo Ndg. George Emmanuel Mbilinyi amemhakikishia Mbunge huyo kuwa atashiriki kikamilifu wakati wa kusimamia ujenzi wa Mradi huo kuanzia hatua za mwanzo hadi utakapokamilika.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.