Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe: Dunstan Kitandula (Mb) amefanya ziara ya kikazi leo tarehe 16/07/2024 katika kata ya Chiponda na Mnala zilizopo Tarafa ya Rondo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ikiwa ni muendelezo wa Ziara yake ya kikazi katika Mkoa wa Lindi kwa lengo la kueleza mipango ya Serikali ili kukabiliana na changamoto ya wanyama waharibifu kama tembo.
Katika Ziara hiyo Mhe: Kitandula alipokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe: Zainabu Tellack, Mkuu wa Wilya ya Lindi Mhe: Shaibu Ndemanga, Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Mtama Ndugu Anderson D Msumba, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama Mhe: Yusuf Tipu, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Mhe: Athumani S Hongonyoko, Madiwani wa kata zote mbili pamoja na Mwenyekiti wa kijiji cha Chiodya.
Akiongea na Wananchi waliojitokeza katika mkutano huo Mhe: Kitandula alisema kuwa kwa mara ya kwanza Serikali imetenga fedha nyingi katika mwaka huu wa fedha ikiwa ni pamoja na kununua Helkopta 2 na matumizi ya ndege nyuki (Drones) ili kupata urahisi wa kukabiliana na wanyama waharibifu lakini pia kuboresha mabomu baridi kwa kuyaongezea kishindo na mwanga ili kufukuza tembo kwa umbali mrefu.
Mhe: Kitandula aliongeza kuwa Serikali imepanga kutoa mabomu baridi 500 katika jimbo la Mtama na kuongeza Askari wengi Zaidi kwa kuwapatia mafunzo na vifaa lakini pia kuwapa mafunzo wananchi walio karibu na hifadhi ili waweze kujilinda na wanyama hao waharibifu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.