Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Dkt. Festo John Dugange ameridhishwa na hatua iliyofikiwa ya upauaji wa majengo mawili katika ujenzi wa kituo cha afya cha Mtama huku akitoa pongezi kwa maendeleo mazuri ya ujenzi huo. Pengezi hizo amezitoa Leo Novemba 26, 2021 akiwa kwenye ziara yake ya kikazi na kuweza kutembelea na kukagua maendeleo ya mradi huo katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.
Akitoa maelezo kuhusu ujenzi huo, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Dismas Masulubu amesema kuwa Halmaahauri ilipokea Tshs. 250,000,0000/= ambapo jumla ya Tshs. 112,000,000/= zimetumika hadi kufikia hatua ya upauaji kwa jengo la OPD pamoja na maabara na kuongezea kuwa kazi inaendelea na kwamba wakati mafundi wanasubiria bati kwa hatua ya uwezekaji jengo la maabara tayari miundombinu ya umeme na madirisha imewekwa.
Licha ya pongezi hizo, Naibu Waziri amewataka viongozi kusimamia kikamilifu kwenye hatua ya kumalizia ( finishing) ili thamani ya fedha iendane na ubora wa jengo husika huku akisisitiza kuwa kumalizika haraka ndio nafasi ya kuongezewa kwa fedha nyingine za muendelezo wa ujenzi wa majengo mengine.
Aidha Dkt. Dugange ametoa ushauri wa kuongeza eneo la akiba litakalotumika kwa matumizi mengine ya kituo miaka kenda ijayo.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri alipata nafasi ya kutembelea Mradi wa ujenzi wa ofisi za Halmashauri ambapo aliridhishwa na uteuzi wa eneo lililotengwa kwa ajili ya Mradi huo kuwa mbali na makazi ya wananchi na kwamba hiyo ni hatua moja wapo ya kuufanya mji kukua kwa kasi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.