Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mhe. Yusuf Abdallah Tipu ambaye pia ni Diwani Kata ya Nyengedi leo Disemba 20, 2021 amefanya ziara ya kikazi ya kutembelea na kukagua Miradi ya ujenzi wa madarasa ya UVIKO-19 yanayoendelea kujengwa katika Halmashauri hiyo . Mhe. Tipu alitembelea Miradi ya Tarafa ya Nyangamara, Sudi pamoja na Rondo huku akionesha kuridhishwa na maendeleo yake lakini pia hakusita kutoa msisitizo kwa mafundi pamoja na wasimamizi wa ujenzi kufanya kazi kwa bidii, ushirikiano na uzalendo wa hali ya juu ili iwe chachu ya kukamilisha miradi hiyo kwa kiwango kinachoendana na thamani ya fedha.
Kwenye ziara hiyo aliambatana na wataalamu mbalimbali wa Halmashauri ikiwa ni pamoja na Ndg. Abruhani Juma ambae ni Mkuu wa Idara ya ujenzi pamoja na Ndg. Salum Mohamed Mpili ambae ni Mkuu wa Idara ya Mipango.
PICHA
Mwenyekiti ( wa kwanza kushoto) akiwa kwenye shule ya sekondari Mnara
Madarasa 3 shule ya sekondari Mnara
kituo shikizi Mkung'uni madarasa 2
kituo shikizi Mnazimmoja
Madarasa 4 shule ya sekondari Madangwa
madarasa 2 kwenye kituo shikizi Pangaboi
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.