Mwenge wa Uhuru ulipokelewa katika Kata ya Madangwa iliyopo ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Lindi tarehe 20/06/2018 ukitokea katika mkoa wa Mtwara na ulitembezwa katika Miradi 7 na moja ya miradi iliyotembelewa na kuzinduliwa ni Mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha kuchakata Mihogo cha CASSAVA STARCH OF TANZANIA CORPORATIVE LIMITED ambacho kitajengwa katika kijiji cha Mbalala, kata ya Majengo, Halmashauri ya wilaya ya Lindi.
Mara baada ya kukamilika kwa ujenzi wa Kiwanda hichi cha kuchakata Mihogo jumla ya vijana zaidi ya 200 wanatarajiwa kuajiliwa katika kiwanda hiki cha CASSAVA STARCH OF TANZANIA CORPORATIVE LIMITED hayo yamesemwa na Mkurugenzi wa utawala na Rasilimali watu ndugu Knowles Lumambo mara baada ya Mwenge wa Uhuru kuzindua ujenzi wa Kiwanda hicho cha uchakatuaji wa Mihogo. Pia ndg Knowles Lumambi (Meneja rsilimali watu) aliongezea katika kuunda mikono jitihada za Raisi wa awamu ya tano Mhe Joseph Pombe Magufuli ya kufikisha nchi katika uchumi wa kati
Tumejipanga katika ujenzi wa viwanda viwili ambavyo kutakuwa na Viwanda vya unga wa muhogo na Wanga,lakini kwa sasa tutaanza na ujenzi wa kiwanda cha unga wa Muhogo ambao unatajia kugharimu kiasi cha dola za Marekani million nne na matayarisho ya eneo la ujenzi tayari yamekwishafanyika na zoezi la kumpata mkandarasi limekamilika,Kiwanda kinatarajiwa kuanza uzalishaji wake November 2018 mwaka huu.
Mkimbiza Mwenge Kitaifa ndg Charles Kabeho mara baada ya kuzunguka maeneo hayo ya uwekezaji ya ujenzi wa kiwanda hicho alimpongeza mwekezaji wa kiwanda hicho kwa kuunga mkono jitihada za serikali kwa mpango wa utekelezaji wa sera ya viwanda na pia alimwagiza Mkuu wa wilaya ya Lindi Ndg Shaibu Ndemanga kuharakisha Wananchi sita(6) kulipwa fidia ya maeneo yao yaliyochukuliwa na Kiwanda na Mkuu wa Wilaya aliahidi kushughulikia fidia hiyo ndani ya Mwezi mmoja na ifikapo tarehe 20/07/2018 wananchi wote watakuwa washalipwa fidia zao.
Mwaka 2018 kauli kuu ya mbiu ya mwenge wa uhuru ni " Elimu ni ufunguo wa maisha wekeza sasa kwa maendeleo ya Taifa letu".
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.