Mkazi mmoja wa kijiji cha Mihogoni kilichopo Kata ya Mtama aliyejulikana kwa jina la Nurudini Shabani mwenye umri wa miaka 19 Alfajiri ya tarehe 4 Novemba, 2021 ameng'atwa na Mbweha wakati akienda kuokota embe katika miembe iliyopo jirani na shule ya Msingi Mihogoni.
Wananchi wenye hasira kali walifanikiwa kumuua Mbweha huyo na kutoa taarifa kwenye ofisi za Idara ya Mifugo Halmashauri ya Wilaya ya Mtama. Wataalamu wa Mifugo wakiongozwa na Daktali wa Wilaya Dkt. Joseph Sijapenda walifika eneo la tukio na kuchukua ubongo kwa ajili ya vipimo vya awali na kugundua kuwa mbweha huyo alikua na virusi vya ugonjwa wa kichaa cha mbwa.
Kijana aliyejeruhiwa amepewa barua ya utambulisho na kupelekwa hospitali ya Ndada ambako matibabu ya ugonjwa huo yanapatikana.
Dkt. Sijapenda ametoa wito kwa wananchi waliojitokeza kwenye eneo la tukio kuhakikisha kuwa na utaratibu wa kuwafungia Mbwa wao kipindi cha mchana na kuwafungua majira ya usiku kwa lengo la ulinzi lakini pia kuwachanja chanjo ya kuzuia ugonjwa wa kichaa cha Mbwa. Aidha, pindi wanapowaona wanyama kama paka, Mbwa, mbweha wana dalili za ugonjwa huo watoe taarifa kwenye ofisi za Idara ya Mifugo na Uvuvi ya Halmashauri ya Mtama au kwa Mtaalamu yeyote wa Mifugo aliye karibu naye.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.