Keelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania yatakayofanyika tarehe 26 Aprili 2024, Wafanya kazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama, Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wananchi wa Mtama wameshiriki katika zoezi la kufanya uasfi wa mazingira na kupanda miti 1000 (miti ya matunda na miti ya mbao) kuzunguka eneo la kituo cha Afya Mtama. Zoezi hilo limefanyika leo tarehe 24 Aprili 2024.
Akiongea na wananchi waliojitokeza katika zoezi hilo Mganga mkuu wa Halmashauri Ndugu Dismas Masulubu aliishukuru Serikali kwakutoa milioni 500 kwa ujenzi kituo hiko na Shilingi milioni 450 kwa ajili ya vifaa tiba, Aidha Ndugu Selemani Livemba Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Lindi aliwashukuru wananchi kwa kujitolea kwa moyo na kufanikisha ujenzi wa kituo hiko.
Aidha Mgeni Rasmi wa tukio hilo Mzee Hongonyoko Mwenyekiti CCM Wilaya ya Lindi alimshukuru Rais Daktari Samia Suluhu Hassani kwa kujenga kituo bora cha Afya na alitumia fursa kupeleka changamoto za wananchi kama vile Ujenzi wa soko, miundombinu ya maji na barabara za Mitaa kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Mzee Hongonyoko aliongeza kuwa Muungano ni urithi na umoja wetu hivyo wananchi wanapaswa kuwa wazalendo na kuutunza Muungano huo. Mkurugenzi Mtendaji aliwashukuru wote walioshiriki hasa wananchi kwa kujitokeza kwa wingi kufanikisha zoezi hilo. Mwisho watu wote walisema kaulimbiu ya maadhimisho hayo "TUMESHIKAMANA NA TUMEIMARIKA KWA MAENDELEO YA TAIFA LETU"
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.