Hayo yamesemwa leo Julai 28 2021 na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Moses Nnauye katika Uwanja wa Mkorosholofa kijiji cha Mihogoni wakati akitolea ufafanuzi wa hoja na maswali yaliyoibuka kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Mvuleni na Mihogoni katika mkutano wa adhara na wananchi hao.
Katika ziara yake hiyo wananchi walipata nafasi ya kuuliza maswali na kutoa mapendekezo yao kuhusu mambo mbalimbali ya kimaendeleo ambapo miongoni mwa hoja na maswali yaliyoibuka na kupatiwa ufafanuzi kutoka kwa Mh. Mbunge ni pamoja na suala la umeme, maji, pamoja na upimaji wa mji.
Akitolea ufafanuzi wa hoja na maswali mbalimbali yaliyoibuka katika ziara yake, Mh Nape ametoa ahadi kuhusu suala la umeme kuwa atalifanyia kazi. "Niwaahidi Kuwa lazima tuongeze nguvu kwenye suala ya umeme ndani ya Jimbo na niwahakikishie tutamaliza tatizo la umeme. Mtama ndio makao makuu ya Jimbo na na Halmashauri hivyo ni lazima tuipe heshima". Alisema Mh Nape Mbunge Jimbo la Mtama katika kijiji cha Mihogoni. Aidha ameendelea kusisitiza kuhusu bei ya umeme ambayo ni 27000Tsh na kwamba nguzo za umeme zitapatikana bure bila Malipo. Sambamba na hilo Mh Nape amesema zaidi ya shilingi bil.5 zimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa miundombinu na miradi ya maji.
Aidha Mh. Nape ametolea ufafanuzi kuhusu ujenzi wa kituo cha afya katika kata ya Mtama ambapo amesema kuwa kituo cha afya kitajengwa katika kijiji cha Mpenda kata ya Mtama. Vilevile amesema serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa shule za sekondari zipatazo sita na moja itajengwa Mtama ikiwa ni shule ya kisasa yenye mabweni kwa lengo la kuinua sekta ya elimu.
Kuhusu suala la upimaji wa mji, amesema kuwa ni zoezi linalohitaji kiasi kikubwa cha fedha hivyo basi kupitia kwa waziri wa ardhi wameomba fedha ili kurahisisha zoezi hilo. Sambamba na hilo amewaomba wananchi kukabiliana na changamoto ya ubomoaji wa baadhi ya majengo na mimea wakati wa zoezi la upimaji wa mji likiendelea.
Mh. Nape amewaomba wananchi wa kata ya Mtama kuweke tofauti za kisiasa Mandi na badala yake kutoa ushirikiano na diwani wa kata ili kupelekea maendeleo, vilevile amemtaka diwani wa kata ya Mtama kuzunguka katika maeneo yake ya kata ili kufahamu changamoto zinazowakabili wananchi wake. Pia ametoa wito kwa vijana kujitokeza kwa wingi kufanya katika miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kujipatia kipato.
Mh. Nape anaendelea na ziara yake ya kikazi katika Jimbo hilo ndani ya Halmashauri ya Mtama ambapo Leo amepata nafasi ya kuzunguka katika vijiji vya Mpenda, Mihogoni, na Makonde kata ya Mtama na kuzungumza na wananchi kuhusu mambo mbalimbali ya maendeleo jimboni hapo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.