Dawa hizo zimesambazwa kufuatia agizo la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Kassim Majaliwa Majaliwa alilolitoa katika ziara yake ya kikazi Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi 5/10/2021 mara baada ya kupokea changamoto ya ukosefu wa dawa kwenye vituo vya kutolea huduma ya Afya na kutoa maagizo kwa Mkurugenzi wa Bohari Kuu ya Madawa (MSD) kuhakikisha kuwa dawa zinasambazwa kwenye vituo mbalimbali.
Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Dismas Masulubu amethibitisha kuwa usambazaji wa dawa hizo umepanda kwa aslimia 82% ukilinganisha na asilimia 35% hadi 40% za awali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama amekemea vikali vitendo vya ubadhirifu wa madawa unaofanywa na baadhi ya watumishi wa Afya na kwamba wakibainika hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao ikiwemo kulipa fedha za Serikali zilizotolewa kwa ajili ya manunuzi ya dawa hizo
Wananchi wametoa shukurani kwa Uongozi wa awamu ya sita chini ya usimamizi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan kwa kutatua changamoto hiyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.