Mafunzo ya HPV yametolewa leo Tarehe 27 Januari 2020 kwa Maafisa Elimu Kata na Wataalamu wa Afya katika Zahanati na vituo vya Afya vyote katika Halmashauri ya Mtama. Mafunzo hayo ya siku yamefanyika katika ukumbi wa mikutano Mtama. Lengo la mafunzo ni kuwawezesha Wataalamu hao kuwapatia kinga hiyo kwa wasichana wote wenye umri wa miaka 14, program hii imeanza 2018 na ni endelevu na inatolewa kila Mwaka kwa lengo la kuwanusuru kupata virusi vya saratani ya shingo la uzazi kwa watoto hapo watakapokuwa watu wazima. Mafunzo hayo yameandaliwa na ofisi ya Mganga Mkuu wa Halmashauri na kusimamiwa na mratibu program wa Mkoa wa Lindi. Baada ya mafunzo hayo utaratibu wa kutoa kinga utaanza Mara moja katika shule za Msingi na Sekondari pamoja na vituo vya Afya na Zahanati.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.