Ukaguzi wa Miradi ya visima vya kuvunia maji ya mvua inayotekelezwa na Wanufaika wa Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini kupitia Mradi wa Ajira za Muda katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama umefanyika leo tarehe 17 Disemba 2021na Mratibu wa TASAF Ndg Cosmas Mwantisya pamoja na Mhandisi Zebedayo Selemani ikiwa ni sehemu ya kujipatia ujira kwa Walengwa hao.
Katika zoezi hilo Mratibu huyo amesisitiza kuongeza kasi ya ujenzi ili kuendana na muda kabla mvua hazijaanza kunyesha kwa mfululizo huku akitoa pongezi kwa kuwa maendeleo ya ujenzi wa visima hivyo upo katika hatua nzuri na kwamba visima vyote vipo kwenye hatua inayofanana na vinatarajiwa kukamilika ndani ya mwezi huu Desemba 2021
Mradi huo unafadhiliwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na una jumla ya visima 22 katika vijiji 13 vilivyomo katika Tarafa ya Mtama, Rondo, Nyangamara na Sudi. Kukamilika kwa visima hivyo vitasaidia kupunguza tatizo la maji kwa wananchi wa maeneo husika.
Wanufaika wa TASAF Ntene wakiendelea na ujenzi wa kisima cha kuvunia maji ya mvua
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.