Katika jitihada za kutambua na kuthamini uwepo wa watoto wenye mahitaji maalumu nchini, Mradi wa TUNANDOTO TANZANIA chini ya usimamizi wa Kanisa la Pentekosti (FPCT) umekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali kwa wanafunzi 49 wenye ulemavu waliopo katika shule ya Msingi Nyangao ili kuwawezesha, kuwapa faraja na matumaini ya kufanya vizuri kwenye masomo yao na kuweza kufikia malengo yao. Vifaa hivyo vimetolewa tarehe 8 Oktoba 2021 na Mratibu wa Mradi huo Mwl. Suleiman Mosses kutoka Ruo Seminari ambapo amekabidhi shuka 100, kofia 17, sukari kg 50, vifaa vya shule, juisi katoni 8, biskuti boksi 2 pamoja na sabuni za kunawia dazani moja.
Akitoa maelezo mafupi ya Mradi Mwl. Suleiman Mosses amesema kuwa Mradi huo unajishughulisha na masuala ya kilimo, elimu pamoja na ujasiliamali na kuongeza kuwa Mradi umetoa vifaa hivyo ili kusaidia kupunguza changamoto zinazowakumba wanafunzi hao. Aidha ametoa shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. George Emmanuel Mbilinyi kwa ushiriki wake katika zoezi hilo huku akiahidi kuendelea kushirikiana katika nyanja mbalimbali.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg George Emmanuel Mbilinyi ameushukuru Mradi huo lakini pia ametoa wito kwa wazazi na walezi wasiwafiche majumbani watoto wenye ulemavu na badala yake watumie fursa ya uwepo wa shule hiyo kuhakikisha wanawapeleka na kupata haki yao ya msingi ya kielimu. Sambamba na hilo, Ndg. Mbilinyi amewakaribisha wadau wengine ndani na nje ya Halmashauri kujitokeza kuwapa faraja wanafunzi hao huku akiendelea kutoa msisitizo kwa walimu kubuni miradi mbalimbali itakayosaidia kujiingizia kipato na kuendesha shughuli ndogondogo za shuleni hapo.
Uongozi wa shule ya msingi Nyangao umetoa shukurani kwa msaada huo kutoka katika Mradi wa TUNANDOTO TANZANIA
Mwl. Suleiman Mosses ( kushoto), Mkurugenzi wa Halmashauri Ndg. George Mbilinyi ( kulia) wakiwavesha kofia wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi.
Baadhi ya Wanafunzi wenye mahitaji maalumu wakiwa kwenye tukio hilo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.