Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mkoani Lindi, Shaibu Ndemanga amewataka wazazi wa Mkoa huo kuwapeleka watoto katika usajili wa masomo ya awali na darasa la kwanza Mapema mwezi wa kumi, kumi na moja na kumi na mbili ili kuepusha uchelewaji unaofanywa na wazazi katika kuwapeleka watoto shuleni suala linalodhorotesha utendaji wa walimu madarasani kwani muda mwingi huwa wakiutumia kufanya usajili ilhali elimu ya awali na darasa la kwanza ni muhimu na humtaka mwalimu kuwa makini darasani.
Akizungumza kwa Niaba ya mkuu wa Mkoa wa Lindi, katika kilele cha siku ya maadhimisho ya elimu ya watu wazima, siku iliyoadhimishwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mkoani Lindi, Ndemanga amewataka wataalamu katika sekta hiyo kushiriki katika usajili wa wanafunzi wa darasa la kwanza ili waweze kutambua ni aina gani wa watoto wanatakiwa kujiunga na elimu ya watu wazima.
Aidha, kutokana na Mkoa kutokuwa na Afisa Elimu wa Elimu ya Watu Wazima, Mkuu wa Wilaya ya Lindi ameiomba TAMISEMI kuwapatia mtaalamu huyo kwani Mkoa umejiandaa kujenga misingi mizuri katika elimu ya watu wazima hivyo mtaalamu huyo akipatikana atasaidia katika mipango ya awali iliyodhamiriwa kupangwa na Mkoa hivi sasa.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.