Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akiambatana Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama Mhe. Abdallah Tipu, Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya Ndg. Othmani Hongonyoko pamoja na wataalamu wa Halmashauri ya Mtama 20/01/2022 amekutana na wananchi wa Kata ya Chiponda kwa lengo la kutambulisha mradi wa ujenzi wa shule ya sekondari ya Kata hiyo.
Amewataka wananchi hao kuondoa tofauti zao za kiitikadi za vyama na badala yake wafanye kazi kwa umoja na mshikamano.
Ametoa rai kwa wajumbe wa kamati ya ujenzi pamoja na jamii kuwa waaminifu, waadilifu lakini pia kutengeneza ulinzi shirikishi wa vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huo.
Amewataka vijana wa Kata hiyo kutumia fursa ya ujenzi huo kufanya kazi za vibarua ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Aidha Mhe. Ndemanga amesema mradi huo umepatiwa Tsh 470,000,000/= kwa ujenzi wa awamu ya kwanza utakaohusisha majengo yafuatayo:
- Madarasa 8
- Maabara 3 za sayansi
- Matundu 20 ya Vyoo ambayo 10 wasichana na 10 wavulana
- Miundombinu ya Kuvunia maji
- Minara 2 ya maji
- Tank moja la chini kwa ajili ya kutunzia maji
- Jengo la kisasa la utawala
- Chumba kimoja cha kompyuta.
Kwa upande wao wananchi wa Kata hiyo wametoa shukurani kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Mama Samia Suluhu Hassan kwa kupeleka mradi huo kwani utasaidia kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shule ya Kata ya Mnara lakini pia shule hiyo itawanusuru watoto hao dhidi ya wanyama wakali kama vile tembo.
Mhe. Tipu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama akizungumza na wananchi
Wananchi Kata ya Chiponda wakiwa kwenye mkutano
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.