• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Ujenzi na Zima Moto
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali Asili
      • Afya
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Nyuki
      • Ununuzi na ugavi
  • Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Utalii
    • Uvuvi
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • PICHA
    • MATUKIO
    • HOTUBA
    • HABARI
  • Mifumo
    • ffars
    • National Sanitation Compaign
      • E-learning
    • Sensa Elimu Msingi
    • Wajasiliamali
    • Government mail System
    • Madeni-Demo

MKUU WA WILAYA YA LINDI AWAONYA WANANCHI WANAOFANYA UHARIBIFU WA MISITU

Posted on: November 7th, 2021

Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh. Shaibu Ndemanga amewaonya wananchi wanaofanya shughuli zao karibu na Misitu ya jamii kuacha mara moja tabia ya kuchoma moto mashamba kwaajili ya maandalizi ya shughuli za kilimo kwani hii inasababisha misitu mingi kuungua na kurudisha nyuma juhudi za Serikali na wadau waliojitoa katika upandaji na usimamizi wa misitu hiyo.

Ndemanga, Ameyasema hayo Novemba 6,2021 katika ziara yake ya kukagua Mradi wa Kuongeza Usimamizi wa Misitu ya Jamii unaotekelezwa na Shirika la Usimamizi wa Misitu Asilia TFCG katika Kata ya Namupa Halmashauri ya wilaya ya Mtama mkoani humo.

Aidha, amewataka wananchi hao kuacha kilimo cha kuhamahama, kuendeleza shughuli ndani ya hifadhi na kusisitiza uwepo wa usimamizi shirikishi katika kudhibiti uharibifu wa mazingira kijijini hapo.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Wilaya  aliambatana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Lindi Ndg. Thomas Safari, Afisa utumishi wa Halmashauri ya Mtama Ndg. Mahmoud Kimbokota pamoja na baadhi ya  Wataalamu kutoka Idara mbalimbali za Halmashauri ya Wilaya ya Mtama.

Ndemanga, alianza kupokea taarifa za maendeleo ya Mradi iliyotolewa na Meneja wa Mradi  Bw. Yahaya Mtonda katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri pamoja na kutembelea Vijiji vilivyofikiwa na Mradi huo. Alitembelea msitu na kitaru cha miti kinachosimamiwa na kikundi cha kuweka akiba cha Namupa chenye miche iliyoota jumla ya 1600. Akiwa kwenye kitaru hicho Mkuu wa Wilaya aliwapongeza wanakikundi hao na kuwashauri waongeze juhudi kupanda miti ya asili kama vile mipingo, mibambakofi na mninga.

Kupitia ziara hiyo, aliupongeza uongozi wa TFCG kwa kufanikiwa kupeleka mradi katika Wilaya ya Lindi hususani kwenye vijiji vya ukanda wa Rondo kwani utasaidia kutunza vyanzo vya maji pamoja na uoto wa asili. Aidha aliwaomba watu wa Shirika hilo kuendelea kutoa elimu kwa jamii kuhusu umuhimu wa kutunza misitu ya hifadhi yenye wanyama pamoja na kuongeza juhudi kubwa za kupanda miti ya asili iliyopotea kwenye misitu mbalimbali  ili iwe fursa kwao kuongeza vivutio vya utalii.

Kwa upande wake Meneja wa Shirika hilo Wilaya ya Mtama Bw. Yahaya Mtonda ameeleza ya kuwa shirika limeamua kuanzisha mradi huo ili kuhimiza utunzaji na uongezaji wa misitu kutokana na uharibifu unaopelekea kusambaa kwa wanyama kama vile Tembo wanaovamia maeneo ya shughuli za binadamu hususani kwenye vijiji vya Rondo na kwamba kwa kufanya hivyo kutaimarisha na kuwafanya  wanyama hao kubaki katika makazi yao.

Mtonda aliongeza kuwa mradi huo pia unasaidia kuanzisha vikundi vya kujasiliamali kama vile ufugaji wa kuku pamoja na vikundi vya kuweka akiba ili kujikwamua kiuchumi.  Aidha mradi huo utahakikisha unaanzisha viaru vya miti ikiwa ni  mikakati ya kuendeleza hamasa za uongezaji wa misitu

Katika kuhakikisha misitu inatunzwa na kupunguza migogoro ya ardhi vijijini, Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili Victor Shau ambaye amezungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama,  amesema yakuwa Halmashauri kwa kushirikiana na wananchi pamoja na wadau wa maendeleo  itahakikisha misitu yote inatunzwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na kijacho. Lakini pia ametoa rai kwa uongozi wa vijiji na Kata kutumia kikamilifu sheria ndogo za  Mpango  wa matumizi bora ya ardhi ili kupunguza migogoro isiyokuwa ya  lazima.

Mwenyekiti wa Kijiji cha Muungao II Kata ya Namupa Rafael Milanzi alitumia fursa hiyo kutoa shukurani kwa Shirika la Usimamizi wa Misitu Asilia kwa kusaidia kuondoa migogoro ya mipaka ya Chiwerere-Muungano, Nndawa-Muungano pamoja na Namupa-Muungano. Lakini pia  kijiji kimefanikiwa kutenga msitu wa nyongeza wenye hekta 525 huku akiuomba uongozi wa mradi kukamilisha taratibu ili msitu huo uweze kutangazwa kwenye gazeti la Serikali kuwa kama kivutio cha utalii.

Mradi huo unaofadhiliwa na World Land Trust ulianza rasmi Julai 2020 na unatekelezwa kwa muda wa miaka 3. Mpaka sasa mradi umevifikia takribani vijiji 10 ambavyo ni Ntene, Chiodya, Namupa, Liganga, Mihima, Nndawa, Chiwerere, Muungano II, Mnamba na Mnara. Mradi umefanikiwa kuanzisha misitu ya hifadhi katika vijiji 8 vyenye jumla ya hekta 17376.91, kuwezesha kuanzisha shughuli za ufugaji wa kuku kupitia vikundi vinavyoendeshwa na mfumo wa vikoba ambapo jumla ya kuku 1033 wamesambazwa, pamoja na  kuondoa migogoro ya mipaka ya ardhi kwenye vijiji mbalimbali vya mradi huo.

Dc Ndemanga akiwa kwenye kitaru cha miti Namupa

Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWQENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA KATA, VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MTAMA. September 16, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA KADA ZOTE September 09, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI MTAMA DC September 09, 2023
  • Angalia yote

Habari mpya

  • KAMATI YA SIASA MKOA WA LINDI YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI HALMASHAURI YA MTAMA

    May 09, 2025
  • DC MWANZIVA AMEITAKA KAMATI YA AFYA HALMASHAURI YA MTAMA KUONGEZA UHAMASISHAJI KWA WANAUME KUHUSU UMUHIMU WA LISHE

    April 29, 2025
  • DC MWANZIVA ASISITIZA KUDUMISHA MUUNGANO LINDI

    April 26, 2025
  • KAMATI YA AFYA YA MSINGI YATOA ELIMU KUHUSU NYONGEZA YA DOZI YA CHANJO YA POLIO HALMASHAURI YA MTAMA

    April 24, 2025
  • Angalia yote

Video

Risala ya utii kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Youtube
  • Mfumo wa Elimu Msingi na Sekondari
  • FOMU YA MAOMBI YA LESENI YA BIASHARA
  • Watumishi Portal

Tovuti Mashuhuri

  • Presidential office and Regional Secretariety
  • Electronic Goverment Agent
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Raisi-UTUMISHI
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Box 328 Lindi

    Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc

    Simu ya mezani: 0222061

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@lindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya ndani
    • Katazo
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.