Akiongea hayo katika Hafla ya kufungua msimu mpya wa kilimo wa 2023/2024 na kupokea mbegu za ufuta. Mkuu wa Mkoa wa Lindi Ndugu Zainabu alisema Serikali imelete mashine za kisasa zautambuzi wa ubora wa udongo hili mazao yalimwe katika ardhi sahihi pia Serikali kupitia TARI-Naliendele imelete tani elfkumi ya mbegu bora ya ufuta hivyo maafisa kiliomo wafanyekazi hili jitihada za serikali zizae matunda.
Ndugu zainabu alitoa maagizo matatu kwa maafisa kilimo kama ifuatavyo moja maafisa kilimo wanapaswa kujitoa kwa kutoa elimu kwa wananchi wa Mkoa wa Lindi juu ya njia bora ya Kufanya Kilimo, pili Maafisa kilimo watapimwa utendaji wao kwa mazao yatayopatikana katika kata zao,tatu Maafisa kilimo wanatakiwa kugawa mbegu ya ufuta kwa wakulima tu pia aliongeza kuwa viongozi wa Halmashauri huska wanapaswa kufuatilia zoezi la ugawaji wa mbegu hizo na kuchukua hatua kali pindi udanganyifu utapopfanyika.
Alkadhalika ndugu Zainabu alipongeza Serikali ya awumu ya sita chini ya Mheshiwa Raisi daktari Samia Suluhu Hassani kwa kuthamini sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji na kuongeza bajeti katika sekta hiyo sambamba na hilo Ndugu Zainabu alitoa salum za pole kwa Halmashauri ya Wilaya ya Hanang kwa maafa yalliyowakuta.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.