Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Zainabu Telack leo tarehe 17, Februari 2024, amefanya kikao na wafanyakazi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtama ili kusikiliza Changamoto, Maoni, na Mapendekezo ya wafanyakazi kwa maslahi ya maendeleo ya Mkoa na Halmashauri, kikao kilifanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmsahuri.
Wafanyakazi waliwasilisha changamoto zao kama vile malipo fedha ya uhamisho, miundominu ya barabara, vyombo vya usafiri, fedha za likizo, wanasiasa kuingalia utendaji kazi, changamoto ya bima ya Afya, uhaba wa Nyumba za Walimu, upungufu wa vyoo mashuleni na umaliziaji wa miradi.
Mkuu wa Mkoa alipokea changamoto hizo nakuzijbu pia aliwataka wakuu wa idara kujibu changamoto zinazohusiana na idara yao, Mkuu wa Mkoa aliendelea kuwa ni vizuri Halmashauri ikafuata ushauri wa wafanyakazi ili kujiongezea kipato kama vile kutanganza sehemu za utalii na kujenga hoteli ya chakula kwa wasafiri.
Pamoja na hayo Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi Ndugu Zuwena Omary alisema kuwa changamoto za wafanyakazi zitasuluhishwa na wafanyakazi wenyewe hivyo wafanya kazi wawe na amani kwasababu changamoto zao zitatatuliwa na alimaliza kwa kushauri wafanyakazi wanapswa kuandaa pensheni yao wakiwa wapo kazini.
Alkadhalika Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Shaibu Ndemanga alimshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwajali wafanyakazi, pia aliongeza kuwa utoro mashuleni ni changamoto kubwa hivyo Halmshauri, wakuu wa shule ya msingi na sekondari, watendaji, makatibu, maafisa elimu, wazazi na walezi wanapaswa kushirikiana kuondoa tatizo hilo.
Mkuu wa Mkoa alisema kuwa wafanyakazi waliopo Mkoa wa Lindi wanabahati kubwa kwasababu Lindi inafursa nyingi, pia alisisitiza wafanyakazi kuwa na uzalendo na umoja wawapo kazini na aliitaka Halmashauri kuwa na mpango mkakati katika kusimamia zao la mbao na magogo.
Mwisho Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Goerge E. Mbilinyi alimshukuru Mkuu wa Mlkoa, Katibu Tawala Mkoa, Mkuu wa Wilaya na wafanyakazi walioshiriki kikao hicho akisema kuwa Halmshauri itafanyia kazi ushauri uliotelewa, baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkuu wa Mkoa alifanya kikao na wakuu wa idara wa Halmshauri ya Wilaya ya Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.