Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Mheshimiwa Yusufu Tipu Leo tarehe 27 Febuari, 2024 ameliongoza Baraza la Madiwani kupitia taarifa mbalimbali kutoka kwenye kata, Mkutano huo umefanyika katika ukumbi wa Halmashauri.
Aidha Waheshimiwa madiwani waliwasilisha changamoto mbalimbali kama vile miundombinu ya barabara, upungufu wa wafanyakazi mashuleni na vituo vya Afya, changamoto ya maji, upungufu wa nyumba za wafanyakazi hasa waalimu hivyo kuwataka wataalamu wa Halmashauri kujibu hoja hizo.
Wataalamu wa Halmashauri walijibu hoja hizo kwa kuelezea mikakati mbalimbali ambayo imepangwa na Halmashauri hili kutatua changamoto hizo, Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi alieleza kuwa Serikali inaendelea kuongeza watumishi katika idara mbalimbali kama ambavyo tulipokea watumishi wapya katika idara ya Afya, kilimo, mifugo na elimu, hivyo Mkurugenzi aliongeza kuwa tutakapo pata watumishi wapya tutafanya msawazo kulingana na uhitaji wa kata husika.
Hata hivyo Mkurugenzi aliishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuboresha maisha ya Watanzania, mwisho Mkurugenzi alisisitiza kuwa yeye ni diwani pia hivyo Waheshimiwa madiwani watumie nafasi hiyo kumfikia na kumpelekea matatizo yao kwa maendeleo ya Mtama.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.