Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi leo Oktoba 8, 2021 amefanya kikao kazi na viongozi wa Idara ya Elimu, Maafisa Elimu Kata, walimu wakuu wa shule za msingi na sekondari kutoka katika shule zote ndani ya Halmashauri. Kikao hicho kimefanyika katika viwanja vya Shule ya Msingi Nang'aka na kujadili mambo muhimu ya kutafuta njia bora ya kuinua na kuendelea Idara hiyo ili kufikia malengo yaliyokusudiwa.
Kupitia kikao hicho, wajumbe walipata nafasi ya kuchangia na kueleza changamoto zinazowakabili kwenye maeneo yao ya kazi huku suala la uhaba wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu, maji, ukosefu wa umeme pamoja na uchakavu wa miundombinu ya shule lilionekana kuwa ni tatizo kubwa kwa shule mbalimbali . Jitihada za kutafuta suluhisho la matatizo hayo, Mkurugenzi huyo alifanya mawasiliano ya papo kwa papo kwa njia ya simu na mamlaka husika ili kufahamu hatua zilizochukuliwa.
Pamoja na hayo, Ndg. Mbilinyi ametoa maagizo kwa wajumbe wa kikao hicho ambayo ni:
Kwa niaba ya wajumbe wa kikao hicho, Muumini Mwinjuma Afisa Elimu Sekondari Wilaya ametoa shukurani kwa nasaha, ushauri pamoja na hamasa zilizotolewa na Mgeni rasmi huku akimuhakikishia kuwa maagizo hayo yanakwenda kufanyiwa kazi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.