Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E. Mbilinyi Leo tarehe 15, February 2024 amezindua rasmi kampeni ya utoaji chanyo ya ugonjwa wa SURUA RUBELLA katika Kituo Cha Afya Mtama chanjo hiyo itatolewa kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na utoaji wa chanyo hizo zitaaza Leo tarehe 15 hadi tarehe 18 Febuari 2024.
Mganga Mkuu wa Halmashauri Daktari Dismas Masurubu alisema kuwa chanyo hiyo itatolewa kwa watoto 18148 na katika Kituo Cha Afya Mtama chanjo hiyo itatolewa kwa watoto zaidi ya 500, aliongeza kuwa Halmashauri imetumia fursa hiyo kutoa chanjo zilizopiata kwa watoto ambao walikosa chanjo hizo, alimaliza kuwa chanjo hizo zitatolewa katika vituo vyote na Halmashauri imeongeza vituo maalumu ili kufanikisha kampeni hiyo.
Mkurugenzi alimshukuru Mheshimiwa Raisi Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kuwajali wananchi kwasababu chanjo hizo zitaenda kuwakinga watoto dhidi ya ugonjwa huo, pia ameawataka wazazi na walezi kuunga mkonon juhudi za Serikali kwa kuwapeleka watoto wao kwenye vituo huska hili wapate chanjo hizo.
Aidha wazazi na walezi walimshukuru Raisi na Serikali kwa kuwajali wananchi kama vile kujenga Kituo Cha Afya Mtama, kutoa chanjo kwa watoto mara kwa mara, upatikanaji wa dawa na vifaa kwenye vituo vya Afya, ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri na waliahidi kwenda kuhamasisha wazazi wenzao kupeleka watoto kupata chanjo hiyo.
Mkurugenzi aliwapongeza wazazi na walezi ambao wamewapelaka watoto wao kupata chanjo hizo na aliwaaomba kwenda kuwaamasisha jamii kuhusu umuhimu wa chanjo hiyo, mwisho aliwataka watoaji wa chanjo hizo kuwa na busara na hekima pindi wanapotoa huduma hiyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.