Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi leo tarehe 5 machi 2024 saa 5 asubuhi ametembelea daraja la Nyangao kwa lengo la kuangalia usalama wa raia na hatua zilizochukuliwa kurudisha Mawasiliano ya barabara iliyokatika eneo la Nyangao katika barabara ya Lindi, Mingoyo na Masasi, Barabara hiyo imeathiriwa na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha ndani ya Halmashauri na maeneo ya karibu.
Aidha Mhandisi Robert Mosea alisema kuwa wameanza kufanya matengenezo ya muda mfupi Ili kurudisha Mawasiliano ya usafiri ndani ya masaa matatu(barabara imeanza kupitika), aliongeza kuwa maji yatakapo pungua ukarabati mkubwa zaidi utafanyika na eneo hilo lipo katika mpango mkakati wa kujengwa daraja kubwa na lakisasa kwa ushirikiano na banki ya Dunia.
Lakini pia Mkurugenzi Mtendaji aliwakilisha salamu kutoka kwa Mkuu wa mkoa na Mkuu wa Wilaya na kuwapongeza wakandarasi hao kwa hatua nzuri waliyo ifikia, mwisho aliwataka wakandarasi kuwasiliana na Halmashauri kama kutatakiwa na usaidizi wa haraka.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.