Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mtama Ndugu George E. Mbilinyi ametembelea mradi wa kituo cha redio Mtama uliopo katika Kata ya Majengo kwa lengo la kuangalia maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo. Redio Mtama itaenda kuwanufaisha wananchi kwa kupata taarifa mbalimbali za Serikali na Halmashauri kwa urahisi pia kuongeza uchumi pindi mradi utakapo kamilika.
Mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Amani amesema kuwa maendeleo ya mradi huo ni mazuri kwani yamefikia asilimia 85 ya utekelezaji ambapo idadi ya vifaa vya kutendea kazi pindi mradi utakapo kamilika vimefikia asalimia 80. Vyumba ambavyo vimekamilika ni chumba cha uzalishaji wa habari,vipindi na matangazo, chumba cha kutunza kumbukumbu na chumba cha studio ambacho ni maalumu kwa watangazaji wa habari na vipindi mbalimbali.
Aidha kutokana na ushauri uliotolewa na TCRA mnamo novemba 2023 ya kuwa jengo la redio linatakiwa kuwa na vyumba nane na Halmashauri iliandaa vyumba vitatu kwa ajili ya mradi huo, hivyo Mkurugenzi amewataka wasimamizi wa mradi huo kuandaa taarifa maalumu ya kuomba jengo lote la ofisi ya Kata ya Majengo litumike kwa ajili ya mradi wa redio na Halmashauri itafute namna ya kupata ofisi mpya ya Kata ya Majengo.
Mwisho Mkurugenzi amemtaka mkandarasi wa mradi huo kuhakikisha anafanya kazi ya viwango vya Juu pia kuongeza choo cha ndani ya jengo la redio ili kuwapa watumishi na wateja urahisi pindi watakapo hitaji kutumia huduma hiyo.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.