Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu George E Mbilinyi leo tarehe 5 machi 2024 ametembelea shule ya msingi Mihogoni, Mtama, Mandawa na Mnolela na kugawa mipira 40 kwa Kila shule kwa lengo la maandalizi ya mashindano ya UMISHUMTA ambayo yataanza hivi karibuni, Mkurugenzi alisema Serikali iliomba mipira kutoka shirikisho la mpira wa miguu Tanzania(TFF).
Afisa Elimu shule za msingi Ndugu Boniface Fungo ameishukuru Serikali kwa kutoa mipira hiyo na huduma mbalimbali wanazozitoa katika shule za msingi ndani ya Halmashauri na kuahidi kuwa Halmashauri itafanya vizuri katika mashindano ya UMISHUMTA.
Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa michezo ina faida mbalimbali kama vile kuimarisha Afya ya mwili na akili, inaleta undugu na ujamaa, michezo ni ajira na michezo inaleta furaha hivyo akaahidi kuwa ataendelea kuunga mkono michezo ndani ya Halmashauri hasa mashuleni, na aliongeza kuwa kwa ushirikiano wetu tutafanya vizuri katika mashindano ya UMISHUMTA.
Pia Mkurugenzi alitumia fursa hiyo kuongea na wanafunzi na kuwauliza maswali mbalimbali alifurahishwa jinsi ambavyo wanafunzi walikua wanajibu maswali hayo kwa kutoa zawadi mbalimbali kama vile mwanafunzi Alawi Ali Nyale kutoka shule ya msingi Mihogoni alipata kiasi Cha fedha elfu 50 kwa kujibu swali vizuri, alitoa zawadi zingine kama pipi na biskuti.
Pamoja na hayo Mkurugenzi Mtendaji alikutana na waalimu wanaojitolea katika shule hizo alipendezwa na moyo wa uzalendo wa waalimu hao lakini pia aliongea nao na kuwashauri mambo mbalimbali yanayohusu kazi yao na aliwapa zawadi kwa lengo la kuwatia moyo. Mwisho aliwataka waalimu wakuu na waalimu wa michezo kutunza mipira hiyo na vifaa vingine vya michezo katika shule zao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.