Ndugu Anderson D Msumba Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama leo tarehe 12 Julai 2024 amefanya kikao na idara ya Afya kwa lengo la kukumbushana mambo mbalimbali yanayohusu idara hiyo,kikao hiko kimefanyika katika ukumbi wa mikutano uliopo Halmashauri ya Mtama.
Akiongea na watumishi hao Mkurugenzi Mtendaji alisema kuwa watumishi wa Umma wanatakiwa kufanya kazi kwa weledi na kuheshimiana kwa nafasi zao ili kutimiza malengo waliyo jiwekea kama idara na aliongeza kuwa maisha ya binadamu yanahitaji Elimu na Afya ili kuendeleza na kukuza uchumi wa Taifa letu kwani mtu mwenye Afya njema ataweza kufanya kazi kwa bidii.
Mwisho aliwataka watumishi wa Afya kuhakikisha wanatoa huduma zilizo bora kwa Wagonjwa kwani huduma inabeba vitu vikuu vitatu ambavyo ni Matibabu, Dawa na Mapokezi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.