Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndugu Goerge E. Mbilinyi ametembelea mradi mkubwa wa maji uliopo Kata ya Mandwanga wenye thamani ya bilioni 3.1 uliofadhiliwa na Kanisa la Angalikana Jimbo la Masasi, mradi huo utaondoa tatizo la maji katika vijiji nane ndani ya kata hiyo yenye jumla ya idadi ya watu elfu 20, mradi huo ulianza kutekelezwa 2022 na utakamilika juni 30, 2024 baada ya kumilika mradi utakabidhiwa kwa RUWASA-Lindi.
Mkandarasi wa mradi huo Mhandisi Olaph John alisema kuwa mradi umegawanywa katika miradi midogo minne ambapo vijiji viwili vimeunganishwa kwenye mradi mdogo mmoja, mgawanyo huo upo kama ifuatavyo Kijiji cha Nyundo I na Kijiji cha Nambahu ni mradi wa kwanza, Kijiji cha Chihuta na Mikongi mradi wa pili, Kjiji cha Mandwanga na Kijiji cha Lindwandwali mradi wa tatu na mradi wa mwisho ni Kijiji cha Malangu na Kijiji cha Mnazi mmoja.Aidha Mhandisi Olaph John aliongeza kuwa hadi kufikia Machi 15, 2024 miradi midogo mitatu itakua imeaza kufanya kazi isipokua mradi mdogo wanne ambao hadi kufika juni 30, 2024 mradi huo utakua umeanza kufanya kazi.
Sambamba na hilo Mkurugenzi alipongeza juhudi zinazofanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania daktari Samia Suluhu Hassan kwa kushirikiana na mashirika mbalimbali kama Kanisa la Angalikana katika kuboresha huduma za jamii hasa maji kwa wananchi na kufikia lengo la kampeni ya kumtua mama ndoo kichwani.
Alkadhalika Ndugu Goerge Mbilinyi ameawataka wananchi wa kata hiyo kuthamini juhudi zinazofanywa na Serikali kwa kutunza miundominu hiyo na waunge mkono juhudi hizo kwa kuvutia maji majumbani kwao pindi mradi utakapo kamilika kwa sababu ghalama zitakua rahisi sana.
Pia Mkurugenzi aliwapongeza wananchi waliokubali kwa ridhaa zao kutoa maeneo yao hili kuwezesha kukamilika kwa mradi huo akisema kuwa Halmashauri itatambua uzalendo wao. Pamoja na hayo Mkurugenzi aliambatana na wajumbe wafuatao kwenye ziara hiyo kama ifuatavyo Afisa Utumishi Ndugu Kalingonji, Afisa Manunuzi Ndugu Chacha, Afisa Mipango Bi. Emma, Afisa Maendeleo ya Jamii na wawakilishi wa Kanisa la Angalikana Jimbo la Masasi.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.