Serikali ya awamu ya sita chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassani kupitia Mpango wa Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano Dhidi ya COVID 19 imepeleka fedha za mkopo wa masharti nafuu kutoka IMF zitakazosaidia kupambana na ugonjwa UVIKO 19 katika Mikoa na Halmashauri mbalimbali nchini.
Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ni Halmashauri iliyoko kwenye mpango wa ujenzi wa madarasa 38 ya shule za sekondari, madarasa 20 ya vituo shikizi. Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imepokea Tshs 1,160,000,000.00/= kwa ajili ya ujenzi wa miradi hiyo inayotekelezwa kwa njia ya force account na tayari utekelezaji wake umeanza kwenye hatua mbalimbali na kazi inaendelea.
Kukamilika kwa Miradi hii kutasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi na kusaidia kutimiza lengo la kujikinga na homa ya mapafu UVIKO 19, lakini pia yatasaidia kupunguza changamoto za uhaba wa madarasa kwa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo 2022, pamoja na kuwasaidia wanafunzi kutotembea umbali mrefu hadi kuzifikia shule zao kutokana na uwepo wa vituo shikizi katika maeneo mbalimbali.
BAADHI YA MADARASA KWENYE HATUA MBALIMBALI:
Mtua sekondari madarasa matatu
Shule ya sekondari Mnolela madarasa manne
Kituo shikizi Mkung'uni madarasa mawili
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.