Hayo yamesemwa na Kaimu Afisa Mipango Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. Nurudini Rweyugenza Januari 2, 2022 wakati akiwasilisha bajeti ya mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye Kikao maalumu cha Baraza la Madiwani ambapo amesema kuwa fedha Tsh Bil. 26 zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya Halmashauri hiyo huku akifafanua kwamba Bil. 23 kutoka Serikali kuu, Mil. 717 fedha za mapato ya ndani ni pamoja Bil. 2 kutoka kwa Wahisani.
Aidha, Ndg. Rweyugenza aliongezea kuwa kupitia fedha Tsh Mil.717 za mapato ya ndani Halmashauri imeweka kipaumbele katika utekelezaji wa Miradi ifuatayo;
1). Uendeshaji wa shughuli za Kilimo kwa Tsh 50,000,000/=
2). Mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu 179,000,000/=
3). Mpango wa kuanzisha kiwanda cha misumari 400,000,000/=
4). Umaliziaji wa Miradi viporo iliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi 30,000,000/= wakati kiasi kilichosalia ni kwa ajili ya ufuatiliaji na usimamizi wa Miradi yote kulingana na Idara husika.
Kupitia Baraza hilo, Meneja wa TARURA Wilaya ya Lindi Eng. Pascal Dauson alipata nafasi ya kusoma bajeti ambapo alisema TARURA kwa mwaka wa fedha 2022/2023 imekusudia kufanya matengenezo ya barabara zenye changamoto kubwa pamoja na kuboresha barabara ambayo tayari zilifanyiwa kazi kwa hatua za mwanzo.
Eng. Dauson aliongeza kuwa barabara ambazo zimepewa kipaumbele kupitia bajeti hiyo ni zile zenye matumizi ya muhimu ikiwa ni pamoja na barabara za kuelekea Hospitali ya Wilaya, ofisi mpya za Halmashauri na maeneo ya uzalishaji mkubwa.
Madiwani wamekubaliana na kuipitisha bajeti hiyo wakiwa kwa matumaini na matarajio ya kuendeleza na kuongeza mapato ya Halmashauri hiyo hususani kupitia mpango wa kuanzisha kiwanda cha misumari.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.