Mbunge wa viti maalaum anaeshughulikia wafanyakazi Mh. Dkt. Alice Karungi Kaijage amefanya ziara ya kutembelea Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa lengo la kusikiliza changamoto, ushauri na mapendekezo ya watumishi wilayani hapo.
Katika kikao kilichofanyika leo tarehe 22 Disemba, 2023 katika ukumbi wa Halmashauri, watumishi wa Halmashauri kwanza waliishukuru Serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshimiwa Raisi Daktari Samia Suluhu Hassan kwa kutoa Mishaara kwa wakati, Kupunguza Kodi ya mshahara, kuripa madeni ya wafanyakazi lakini pia juhudi za Serikali kupandisha madaraja watumishi. Pili walitoa changamoto zao kama ifutavyo Serikali kuongeza mshahara, Serikali kupunguza kodi ya mshahara, Serikali kuwaendeleza watumishi kielimu, Serikali kutatua taharuki ya kikokotozi, changamoto ya utegemezi wa bima ya afya, kulipwa kwa wakati malipo ya likizo, kupandishwa madaraja, kubadili muundo wa upandishaji madaraja pamoja na ongezeko la fedha ya matumizi mengineyo (OC).
Mhe. Kaijage alipokea pongezi za watumishi kwa Serikali ya awamu ya sita na kujibu changamoto mbalimbali za watumishi na kuhaidi kuchukua changamoto hizo na kuzipeleka ngazi za juu. Aidha suala la kikokotozi Mhe. Kaijage alisema kuwa Raisi aliomba aachiwe suala hilo hivyo watumishi watulie kwa kuwa Raisi anafanyia kazi suala hilo.
Mhe. Kaijage aliongeza kuwa utegemezi wa bima ya afya ni changamoto iliyojirudia katika Halmashauri nyingi alizopita hivyo ataenda kuishauri idara ya afya kufanya ziara katika Halmashauri ili watoe elimu juu ya bima ya afya kwa wote, utegemezi wa bima ya afya lakini pia wasikilize changamoto na mapendekezo ya watumishi kuhusu bima ya afya.
Pamoja na hayo Mhe. Kaijage aliongeza kuwa ni jukumu lake kuhakikisha kuwa anatekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), akisifu kuwa katika miaka miwili na miezi nane Serikali ya Awamu ya sita imeweza kupandisha madaraja watumishi 425,000 ambapo kwa mwaka inagharimu Serikali shilingi Tilioni 1.12 sambamba na hilo kwa upande wa ajira takribani watumishi 129,000 kutoka Serikali Kuu na 21,000 kutoka Serikali za Mitaa wameajiriwa.
Mhe. Kaijage aliongeza kuwa katika Sherehe za Meimosi zilizofanyika mwaka huu Raisi alisema kuwa taifa lolote linaloendelea chini yake kuna nguvu ya watumishi maneno hayo yanadhihilika katika bajeti ya mwaka wa fedha 2023/2024 ambapo Serikali imeweza kuajiri watumishi 47,000 na kusema kuwa Serikali imeendelea kuwajali watumishi kwa kubadilisha miundombinu ya watumishi 3,345.
Alkadhalika Mhe. Kaijage aliipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Mtama kwa kuwajali na kuwalipa watendaji wa kata na vijiji. Mhe. Kaijage alimaliza kwa kuishauri Halmashauri kuwa na utaratibu wa kufanya kikao mala kwa mala ili kutambua changamoto na kufanya suluhisho za changamoto hizo kwa wakati.
Afisa utumishi wa Halmashauri ndugu Kalingonji kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama ndugu Goerge Mbilinyi alimshukuru Mhe. Kaijage kwa ziara na hotuba yake mzuri kwa watumishi, ndugu Kalingonji aliongeza kuwa Halmashauri imepokea ushauri wa Mhe. Kaijage hivyo Halmashauri itaweka utaratibu sahihi wa vikao pia itaendelea kutatua changamoto za watumishi hasa watendaji wa kata na vijiji.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.