Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi ameotoa wito kwa Maafisa Elimu Kata, Wakuu wa shule za msingi pamoja na sekondari juu ya ubadhilifu wa fedha kwenye usimamizi wa miradi mbalimbali ya kimaendeleo.
Wito huo ameutoa leo Oktoba 25, 2021 wakati wa kikao kazi na wakuu wa shule zote shule za msingi na Sekondari ndani ya Halmashauri katika viwanja vya Ofisi za Idara ya Elimu Nang'aka - Mtama. Sambamba na wito huo, Mkurugenzi ametoa maelekezo kwa wadau hao kusimamia miradi ya ujenzi wa vyumba vya madarasa na vyoo kwa UADILIFU NA UZALENDO wa hali ya juu, kupunguza gharama za matumizi yasiyo leta tija, kuwa wabunifu katika kuleta maendeleo katika maeneo yao ya kazi. Aidha amesisitiza kuwa na mahusiano mazuri baina yao pamoja na wanaowaongoza.
Kwa upande wake Kaimu Muhandisi wa Ujenzi wa Wilaya Eng. Abruhani Juma alipata nafasi ya kutolea ufafanuzi wa namna ya utekelezaji wa miradi hiyo ambapo amesisitiza zaidi kuwa makini kwenye manunuzi ya vifaa vya ujenzi ili kupata miradi inayoendana na thamani ya fedha zilizotolewa
Jumla ya Tshs 760,000,000/= zimetolewa kwa Elimu sekondari za ujenzi wa vyumba vya madarasa huku Tshs 300,000,000/= ujenzi wa shule shikizi madarasa 19, 120,000,000/= madarasa 6 na Tshs milioni 19.8 ujenzi wa matundu 18 ya vyoo kwa baadhi ya shule za msingi. Fedha hizi zimetoka Serikali kuu kupitia Mpango wa Lipa kwa Matokeo (EP4R) na COVID 19.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.