Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi leo 6 Ocktoba 2021 amekutana na kuzungumza na viongozi wa Vyama vya Msingi pamoja na viongozi wa Ghala la kuu la Lindi Farmers Limited lililoko Mtama ili kutoa mwongozo wa usimamizi mzuri wa zao la Korosho kutoka kwa Mkulima hadi kumfikia mnunuzi na kwamba kwa kufanya hivyo kutaimarisha Vyama vilivyopo ndani ya Halmashauri na kuleta ushindani nzuri katika soko.
Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri na kuhudhuriwa na Mbunge wa Jimbo la Mtama Mh. Nape Mosses Nnauye, Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. Yusuf Abdallah Tipu, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ambae alikua Mwenyekiti wa kikao pamoja na Mtendaji wa Bodi ya usimamizi wa Stakabadhi Ghalani Ndg. Asangye Bangu.
Miongoni mwa maelekezo aliyoyatoa Mkurugenzi wa Halmashauri kwa viongozi hao ni pamoja na:
Lakini pia wajumbe wa kikao walipata nafasi ya kujadili changamoto zinazowakabili katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwa ni pamoja na udanganyifu wa Mzani mdogo wa Tani 5 huku Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Ndg. George Mbilinyi akitoa agizo kwa Afisa Ushirika na Mwendesha Ghala la Farmers kulipatia suluhisho suala hilo.
Viongozi wa Vyama vya Msingi wakiwa kwenye kikao hicho.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.