Katika uitikio wa Agizo kutoka Kwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe John Pombe Magufuri, Halmashauri ya Wilaya ya Lindi imeendelea kutekeleza jambo hilo kwa Vitendo mara baada ya Kupokea Vifaa vya Kutunzia na kusafirisha taka kutoka kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii NSSF Mkoa Lindi, Vifaa Hivyo ambavyo ni Mapipa makubwa mawili ya Kuhifadhia Taka na Toroli yaliweza kukabidhiwa hapo jana tarehe 24/04/2018 kutoka kwa Mwakilishi wa Meneja wa NSSF Mkoa wa Lindi Bi Rita Kolowa
Afisa Mazingira wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi Ndg Ismaili Mbani aliweza Kupokea Vifaa hivyo vya Usafi kutoka kwa Bi Kolowa akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Lindi na alimwakikishia kuwa vifaa hivi vya usafi vitatumika kwa Lengo lililokusudiwa la kuweka Halmashauri yetu katika Hali safi na Miongoni mwa Malengo tuliojiwekea ni kufanya Halmashauri hii kuwa ya Mfano wa kuigwa kwa Halmashauri zote nchini
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Lindi Ndg Samwel W Gunzar ametoa Shukrani za dhati kwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya NSSF kwa kuthamini na kuona umuhimu wa kipekee kwa kutoa vifaa hivyo vya usafi na amehakikishia kuwa vifaa hivyo vya Usafi vitatumika kwa lengo lililokusudiwa na kutoa Hamasa kwa Wananchi kujenga tabia ya kufanya Usafi kila Mwisho wa Mwezi kwani kufanya hivi tutaeza kuepukana na Magonjwa yanayosababishwa na uchafu ikwemo kipindupindu na Magonjwa ya Tumbo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.