Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama Ndg. George Emmanuel Mbilinyi akiambatana na Afisa Elimu Sekondari Wilaya Mwl. Muumini Mwinjuma ametembelea shule ya sekondari Mahiwa kwa lengo la kuwapa faraja wanafunzi walioathirika na janaga la moto uliotokea tarehe 26/ 9/ 2021 pamoja na kuwakabidhi sare za shule wanafunzi hao.
Katika hotuba yake, Ndg. Mbilinyi amewataka wanafunzi hao kutokata tamaa na badala yake waongeze juhudi kwenye masomo yao, lakini pia amegusia suala la usalama maeneo ya shuleni ambapo ametoa wito kwa wanafunzi pamoja na walimu kuwa na ulinzi shirikishi ili kujikinga na majanga mengine yasijitokeze zaidi.
Mkurugenzi huyo amekabidhi mashati ya shule 84 huku wanafunzi hao wakitoa shukurani kwa msaada walioupata na kuahidi kufanya vizuri kwenye masomo yao.
Mkurugenzi Ndg. George Mbilinyi ( kulia) akitoa maelekezo kwa Mkuu wa Shule ya sekondari Mahiwa Mwl. Honorati Tarimo
Mwanafunzi wa kidato cha kwanza ambaye ni muathirika wa janga la moto huo akipokea shati la shule kutoka kwa Mkurugenzi
Bweni la wavulana lililoungua moto
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.