Siku ya Malaria Duniani ni maadhimisho ya kimataifa yanayoadhimishwa kila mwaka ifikapo Aprili 25 ili kutambua juhudi za kimataifa za kudhibiti Malaria, kufuatia maadhimisho hayo Ndugu Marcelina Mangula Kaimu Mratibu wa Malaria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama amethibitisha kupungua kwa maambukizi ya malaria kwa 8.2% kutoka 16.8% mwaka 2022 hadi 8.6% mwaka 2023.
Kupungua kwa Maambukizi hayo ni kutokana na juhudi mbalimbali zinazofanywa na serikali ya awamu ya sita chini ya Mheshiwa Rais daktari Samia Suluhu Hassani ambapo mwaka 2023 Halmashauri ilipokea kutoka Serikali kuu viatilifu lita 700 na chandarua 12,000 ili kupambana na maambukizi ya malaria.
Pia Mratibu alisema kuwa taasisi zisizo za serikali kama vile PMI DHIBITI MALARIA walifanya uelimishaji kwa njia ya maigizo kuhusu ugonjwa wa Malaria kwa kata 4 ndani ya Halmashauri na taasisi ya ROTARY CLUB OF KCMC waliweza kufanya mafunzo kwa wahudumu wa Afya ngazi ya jamii kuhusu Ugonjwa wa Malaria na kugawa baiskeli 20 kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii na kugawa vyandarua 1000 kwa Halmashauri kwa ajili makundi maalumu(watoto chini ya miaka 5, wajawazito, wazee na walemavu).
Idara ya Afya itaendelea kufanya kampeni za uhamasishaji katika ngazi ya vijiji na vitongoji kuhusu usafi wa mazingira ili kuondoa mazalia ya mbu, matumizi sahihi ya chandarua, sio kila homa ni malaria nenda kapime na kuwashauri wajawazito kuwahi kiliniki na kupata dawa kinga za malaria.
Mwisho ili kufikia lengo la Zero Malaria ifikapo mwaka 2030 ni lazima wananchi waunge mkono juhudi zinazofanywa na Serikali, ZIRO MALARIA INAANZA NA MIMI NACHUKUA HATUA KUITOKOMEZA.MTAMA BILA MALARIA INAWEZEKANA.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.