Maandhimisho ya upandaji miti kimkoa yamefanyika leo tarehe 20 machi 2024 katika jengo la Halmashauri lililopo katika kata ya Majengo ambapo viongozi mbalimbali kutoka ngazi ya Wilaya na mkoa wamehudhuria zoezi hilo, Viongozi hao ni pamoja na Katibu Tawala mkoa, Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mtama, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama, Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi na wakuu wa idara mbalimbali.
Kaimu Mkurugenzi Halmashauri ya Mtama Ndugu Rashidi Makujunga aliwasisitiza wananchi pamoja na viongozi mbalimbali kuisimamia miti iliyopandwa leo ili iweze kukua vizuri na kuhakikisha nia ya Serikali inafikia malengo yake kwa maendeleo ya Taifa kwa ujumla.
Mgeni Rasmi wa zoezi hilo Mheshimiwa Majid Myao kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya alisema kuwa miti ina umuhimu na matumizi makubwa kwani miti ni biashara, miti ni uchumi lakini pia miti inalinda ardhi yetu dhidi ya majanga kama vile upepo mkali hivyo watu wanaweza kujiajiri kwa kupanda miti hasa ya mbao.
Akiongea na wananchi Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Lindi Mheshimiwa Athumani Sefu Hongonyoko alisema kuwa tunatakiwa kupanda miti kwa ajili ya maisha yetu kwani miti inalinda maisha ya watu ya Kila siku pia Mwenyekiti alikabidhiwa miti 250 na kuahidi kuitunza miti hiyo.
Lakini pia Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mtama Ndugu Yusufu Tipu alisisitiza kuwa tahasisi zote zihakikishe zoezi la upandaji miti linaendelea na kuwa kama utaratibu wa maisha yetu na ameahidi kuitunza miti iliyopandwa leo katika jengo la Halmashauri, Mwisho viongozi pamoja na wananchi walipanda miti katika mashimo maalumu yaliyo andaliwa kwa ajili ya zoezi hilo lakini pia Viongozi waligawa miti kwa Wananchi na kuwashukuru kwa kujitokeza kushiriki zoezi hilo maalumu.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.