• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua pepe |
    • Malalamiko |
Mtama District Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Ujenzi na Zima Moto
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Fedha na Biashara
      • Maji
      • Maendeleo ya jamii, Jinsia na Watoto
      • Kilimo Umwagiliaji na Ushirika
      • Ardhi na Mali Asili
      • Afya
      • Utawala na Utumishi
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Nyuki
      • Ununuzi na ugavi
  • Uwekezaji
    • Viwanda
    • Kilimo
    • Utalii
    • Uvuvi
    • Madini
  • Huduma Zetu
    • Huduma za Afya
    • Kilimo
    • Elimu
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya Waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
    • Ratiba
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Fomu
    • Taarifa
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • PICHA
    • MATUKIO
    • HOTUBA
    • HABARI
  • Mifumo
    • ffars
    • National Sanitation Compaign
      • E-learning
    • Sensa Elimu Msingi
    • Wajasiliamali
    • Government mail System
    • Madeni-Demo

SELEMANI MATHEW AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO

Posted on: August 15th, 2021

Mdau wa michezo Ndg Selemani Methew Luwongo amekabidhi vifaa vya michezo vyenye thamani ya shilingi milioni 4 na laki 6 kwa timu zilizoshiriki na  baadhi ya timu za mpira wa miguu za Mtama . Vifaa hivyo ni pamoja na  jezi za netball na mpira wa miguu, mipira na nyavu za magoli  amevigawa leo tarehe 15 Agosti 2021 katika Bonanza la 'NANI KAMA MAMA TOURNAMENT' katika viwanja vya Bomeni Mtama.

Bonanza  hilo liliandaliwa na kuratibiwa na mdau wa michezo kwa kushirikiana na viongozi wa michezo wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo afisa michezo Wilaya ya Mtama Masoud Mohamed Elewa pamoja na  Walimu wa michezo shule za msingi na sekondari. Washiriki wakuu wa bonanza hilo walikua timu ya netball ya Veterani ya kata ya Majengo na Mtama, Timu ya netball Ya Dada's kata ya Mtama,  timu ya netball ya Mtama sekondari, timu ya netball Mahiwa sekondari,  timu ya netball ya shule ya msingi Mihogoni  na timu ya netball shule ya msingi Mtama na michezo mbalimbali ilichezwa, huku lengo kuu  likiwa ni kuibua, kukuza na kuendeleza  vipaji na michezo ya wanawake pamoja na kuleta hamasa na kujenga afya bora miongoni mwao.

Washiriki wa bonanza wakiburudika

Kabla ya kukabidhi vifaa hivyo, mdau huyo wa michezo alipata nafasi ya kuzungumza na washiriki ambapo amesema kuwa lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuhakikisha halmashauri ya wilaya ya Mtama inakua zaidi kimichezo pamoja na kuibua vipaji mbalimbali katika jamii. Aidha  Ameahidi kufufua na kurekebisha viwanja vya michezo ili viwe katika hadhi ya viwanja vya kiwiilaya hivyo basi amesistiza zaidi kwa washiriki wa bonanza hilo kuithamini na kuipenda michezo kwani michezo ni ajira lakini pia ni njia bora ya kuimarisha afya zao. Sambamba na hayo Ndg Luwongo ametoa wito kwa wenyeji na wadau wengine Wa michezo wajitokeze kwa wingi ili kuwezesha kusonga mbele katika sekta ya michezo.

Nae Afisa michezo Wilaya ya Mtama Masoud Mohamed Elewa ameahidi kufufua na kuendeleza michezo kupitia uwanja huo wa Bomeni lakini pia ametoa wito kwa washiriki wote waliopatiwa vifaa vya michezo kuvitunza vifaa hivyo ili vitumike katika siku zijazo.

Zoezi la ugawaji huo wa vifaa vya michezo litaendelea katika tarafa mbalimbali ndani ya Halmashauri ikiwemo tarafa ya Sudi, Rondo, pamoja na tarafa ya Nyangamara.


Matangazo ya Kawaida

  • TANGAZO LA KUITWA KWQENYE USAILI September 27, 2024
  • TANGAZO LA MIPAKA YA KATA, VIJIJI NA VITONGOJI HALMASHAURI YA WILAYA YA MTAMA. September 16, 2024
  • MATOKEO YA USAILI KWA KADA ZOTE September 09, 2023
  • MATOKEO YA USAILI WA WATENDAJI MTAMA DC September 09, 2023
  • Angalia yote

Habari mpya

  • KAMATI YA SIASA MKOA WA LINDI YATEMBELEA NA KUKAGUA MIRADI HALMASHAURI YA MTAMA

    May 09, 2025
  • DC MWANZIVA AMEITAKA KAMATI YA AFYA HALMASHAURI YA MTAMA KUONGEZA UHAMASISHAJI KWA WANAUME KUHUSU UMUHIMU WA LISHE

    April 29, 2025
  • DC MWANZIVA ASISITIZA KUDUMISHA MUUNGANO LINDI

    April 26, 2025
  • KAMATI YA AFYA YA MSINGI YATOA ELIMU KUHUSU NYONGEZA YA DOZI YA CHANJO YA POLIO HALMASHAURI YA MTAMA

    April 24, 2025
  • Angalia yote

Video

Risala ya utii kwa Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Video zaidi

Kurasa za Haraka

  • Youtube
  • Mfumo wa Elimu Msingi na Sekondari
  • FOMU YA MAOMBI YA LESENI YA BIASHARA
  • Watumishi Portal

Tovuti Mashuhuri

  • Presidential office and Regional Secretariety
  • Electronic Goverment Agent
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Ofisi ya Raisi-UTUMISHI
  • Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya mahali

Wasiliana nasi

    Box 328 Lindi

    Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc

    Simu ya mezani: 0222061

    Simu ya mkononi:

    Barua pepe: ded@lindidc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya ndani
    • Katazo
    • Ramani ya Eneo

Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.