Uzinduzi huo umefanyika Tarehe 13 Machi 2020 katika Kijiji cha Mnara Tarafa ya Rondo. Uzinduzi huo umeenda sambamba na zoezi la upandaji miti lenye kauli mbiu isemayo "Tanzania ya kijani inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya viwanda" akiwahutubia wananchi wa Mnara Mhe, Godfrey Zambi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, aliwaeleza wananchi kuwa Mkoa unazindua leo zao la mkakati katika kuongeza kilimo cha mazao ya biashara licha ya korosho na ufuta. Hivyo tumieni fursa hii kwa kulima zao la KAHAWA aina ya Arabika ambalo litalimwa katika Wilaya za Lindi, Kilwa, Ruangwa na Nachingwea kulingana na hali ya hewa rafiki kwa zao hili. Aidha alisisitiza kutunza mazingira, kupanda miti ya matunda kwa kila Kaya na kila Halmashauri kuwa na kitalu Cha miti. Na aligawa miti ya kupanda kwa wananchi, ekari zaidi ya 450 zinafaa kulimwa zao la KAHAWA katika Mkoa wa Lindi. Mwisho aliwaagiza wazazi kusomesha watoto wao.
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.