Katika harakati za kufikia kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yanayofanyika kila mwaka tarehe 8, Machi, Idara ya Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Mtama imefanya ziara katika shule tatu za Sekondari kwa lengo la kugawa taulo za kike ikiwa ni kuonesha kumjali na kumthamini mtoto wa kike.
Shule walizotembelea ni shule ya sekondari Mtama, Nyengedi pamoja na Kiwalala ambapo walitumia fursa hiyo kutoa elimu ya jinsia, ukatili wa kijinsia na elimu ya UKIMWI.
Taulo hizo zimetolewa kwa walimu wa malezi ili ziwasaidie watoto wa kike pindi wanapopata hedhi wakiwa shuleni.
Wakizungumza Kwa niaba ya wanafunzi wa shule hizo, walimu wa malezi wametoa shukurani kwa watumishi hao juu ya wito wa kutoa taulo hizo kwani zinakwenda kupunguza hali ya utoro unaosababishwa na baadhi ya wanafunzi wa kike kuwa katika siku zao huku wakikosa vifaa vya kujisitiri.
Wanafunzi wa shule ya sekondari kiwalala wakipokea taulo hizo
Wanafunzi wa shule ya sekondari Mtama wakipokea taulo hizo
Wanafunzi shule ya sekondari Nyengedi wakipokea taulo hizo
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.