Mashindano ya Michezo kwa Shule za Sekondari yalianza rasmi mnamo tarehe 26/05/2018 siku ya Jumamosi na yalifanyika katika Viwanja vitatu tofauti ikiwemo Kiwanja cha Shule ya Sekondari ya Lindi,Kiwanja cha Ilulu Stadium na kiwanja cha Kata ya Mtanda na yaliwakilisha Wanafunzi/Washiriki kutoka katika Halmashauri sita za Mkoa wa Lindi ambazo ni Manispaa ya Lindi,Halmashauri ya Wilaya ya Lindi,Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa,Halmashauri ya Liwale,Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea na Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa.
Jumla ya Washiriki/Wanafunzi 482 waliweza kushiriki katika Mashindano haya wakitoka wilaya mbalimbali ikiwemo 112 washiriki/Wanafunzi walitoka katika Shule zilizopo Manispaa ya Lindi,59 washiriki hawa walitoka Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, 85 walitoka Wilaya ya Ruangwa,60 Wilaya ya Liwale,70 wilaya ya Kilwa na 96 washiriki walitoka Wilaya ya Nachingwea, Mashindano haya yalijumuisha michezo Mbalimbali ikiwemo Mchezo wa Mipira ya Miguu, Mpira wa Pete, Mpira wa Meza, Riadha za Mibio mbalimbali Fufi na Ndefu.
Lengo kuu la Mashindano haya ni kuweza kuchuja washindani hawa na kupata timu moja katika kila Mchezo ambayo ndiyo itawakilisha Mkoa wa Lindi kwenye Mashindno ya Kitaifa ambayo yanatarajia kuanza mnamo tarehe 02/06/2018 mkoani Mwanza
Box 328 Lindi
Sanduku la Barua: 328 Lindi Dc
Simu ya mezani: 0222061
Simu ya mkononi:
Barua pepe: ded@lindidc.go.tz
Copyright ©2021 Mtama District Council All rights reserved.